Leo April 8, 2016, Mahakama kuu kanda ya Mwanza imetangaza maamuzi ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge iliyofunguliwa na Ezekiel Wenje tangu 25.11.2015, aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana kutaka Mahakama kupitia upya mchakato wa kujumlisha Matokeo ya Uchaguzi Mkuu October 2015 kati yake na Mbunge wa sasa Stanslaus Mabula, Shauri hilo lililokuwa linasikilizwa na Jaji Kakusuro Sambo kwenye Mahakama Kuu kanda ya Mwanza.
Mahakamani kabla ya kesi kusikilizwa
Mawakili kazini, kabla ya kuanza kusikiliza kesi.
Maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ni kwamba wajibu maombi hawana kesi ya kujibu kwa kuwa mleta Shauri hana ushahidi wa kuithibitishia Mahakama kwamba matokeo yaliyotangwazwa sio halali,Angalia picha za tukio zima.
Katibu wa CCM Mwanza Miraji Mtaturu na Mbunge Stanslaus Mabula, kwenye shangwe
Wanachama wa CCM kwenye shangwe na Mbunge wao.
Post a Comment